Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
George Simbachawene amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanafanya
kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
utumishi wa umma, sambamba na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye
utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma, Simbachawene amesema watumishi hao wanatakiwa kuwa na utendaji unaojali matokeo na kuepuka utendaji wa mazoea.
Amesema
wanatakiwa kuzingatia nidhamu na utendaji wa Watumishi wa Umma,na
watambue maadili ni nguzo muhimu ya kuepuka vitendo vya ubadhilifu na
rushwa mahali pa kazi.
Hata
hivyo, amesema kwasasa inafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa kwenye
ofisi hiyo zinazotokana na uhamisho, upangaji wa walimu na michakato ya
teuzi mbalimbali.
Waziri
huyo amesema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na
vitendo vya rushwa na kwamba watumishi watakaobainika kujihusisha na
vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Sambamba
na hilo, ametaka kila Idara na kitengo kuhakikisha kuwa zinapunguza
matumizi yasiyo ya lazima ili kuelekeza rasilimali fedha katika
kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yataleta tija kwa Taifa.
Simbachawene
amewaambia wafanyakazi hao kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi
ya wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akifafanua jambo
kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Viongozi wa juu na kuwatumikia wananchi
kwa kupunguza changamoto zilizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,
mara baada ya Waziri wa Nchi kushoto kwake George Simbachawene kutoa
hotuba yake kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa
Hazina ndogo mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi George Simbachawene akitoa hotuba kwa Baraza la Wafanyakazi
lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wanaounda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni