Aliyewahi
kuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mzee Yusufu Makamba asema Rais Magufuli anafanana na Yohana
Mbatizaji kwa vile ni kiongozi anayefanyakazi bila kuogopa.
Makamba ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hizi. Alisema
kuwa Rais ni kiongozi mchapakazi ambaye hayumbushwi na maneno wala
vitisho kwa vile anasema ukweli katika kutekeleza majukumu yake.
“Yohana
Mbatizaji alisema ukweli na hakutikiswa na upepo, hakuogopa macho ya
watu wala hakuwa mtu wa majigambo, kama ilivyoandikwa katika Biblia
Takatifu Marko 6:12, na hivyo ndiyo navyomfananisha Rais wetu Magufuli
na viongozi wote tumuunge mkono” alisema Makamba.
Aidha,
kuhusu miaka 55 ya Uhuru , alisema kuwa ni vyema
Watanzania wakazingatia wito wa uhuru ni kazi, na kwa kuwa Serikali hii
imeweka mkazo katika ufanyaji kazi.
Makamba alisema
kuwa katika Awamu hii ya HAPAKAZI TU, inaakisi wito wa Uhuru katika
vipindi mbalimbali kuanzia kipindi cha Uhuru ni kazi na Uhuru na kazi
mara baada ya kupatikana kwa Uhuru na kuwakumbusha watanzania kuulinda
Uhuru.
“Ni
lazima kuulinda Uhuru kwa gharama yeyote ili amani na mshikamano
uendelee kuwepo basi hatuna budii kuepuka lugha zenye maneno ya
uchochezi, ukabila na udini” alisema Makamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni