Wanakijiji
wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi
wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani
Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma,
wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.
Bi
Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga,
wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo,
Desemba 22, 2016.
“Nia
ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia
wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya
kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema.
Alisema,
kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la
Umeme, TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa
Wakala wa Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi
huu wa Backbone kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu
ya umeme na kwa bei nafuu.” Aliongeza.
Alisema,
Serikali kupitia TANESCO imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia umeme
wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya wananchi wa Tanzania
wamepatiwa huduma ya umeme.
Akizungumzia
kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara
na njia za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza
na kusambaza umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme,
Mhandisi Oscar Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha
umeme wa msongo wa Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka
mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma,
umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa kuwasha kipande kilichokuwa
hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.
Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, akizungumza kwenye kituo cha Kibaoni Singida
Mkuu wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kibaoni mkoani Singida, akitoa maelezo kwa wahariri.
Mhariri wa Star TV, Jenifer Sumi
Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akinakili maelezo ya kiufundi kuhusiana na kituo cha umeme cha Kibaoni mkoani Singida.
Picha ya pamoja ya wahariri na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Singida





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni