Akiwasilisha salamu za shukrani kwa mapokezi mazuri aliyopatiwa toka alipowasili Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa, Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa ambayo alipendelea sana kufanya kazi kutokana na uwepo wa fursa nzuri za maendeleo, mandhari nzuri na hali nzuri ya hewa.
”Nimefurahi sana kuwa katika Mkoa huu kwani kwa kipindi chote nilitamani sana kufanya kazi katika MKoa wa Njombe na nilitamani sana kama nafasi hii niliyoipata ningeipata kipindi nilipokua kijana lakini bado nafuraha kubwa kwani ndoto yangu ya kuitumikia na kuifanya Njombe ya maendeleo imeanza kutimia kupitia uteuzi wa Mhe. Rais na ninawahakikishia kuwapatia ushirikiano wa kutosha katika yale yote mtakayoona yanahitaji uwepo wangu.”alisema Mhe.Ole Sendeka.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher ole Sendeka akisalimiana na Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt Samwel Ndalio Thomas mara baada ya
kuwasili Halmashauri hapo. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi
na mweka hazina wa Halmashauri.
Mhe. Ole sendeka akisalimiana na Karani wa Fedha “Cashier” wa Halmashauri Neema Kalundwa
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda akisoma taarifa ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri zilizofanyika.
Mhe.
Ole sendeka akionesha nakala ya kitabu cha Ilani ya uchaguzi ambapo
amewataka watumishi kuisoma na kila mmoja kuwajibika kwenye eneo lake
la utekelezaji kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama Cha
Mapinduzi.Kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson
Saitabahu akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni