Profesa
Ndalichako amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
mdahalo kuhusu kujenga na kukuza maadili ,haki za binadamu,
uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa katika ukumbi wa
makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
“maadili
na makuzi kwa vijana hasa wanafunzi ni suala linalopewa kipaumbelena
serikali ya awamu ya tano hivyo nina imani mdahalo huu umeandaliwa
kuzingatia dhana ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala
mbalimbali hivyo wanafunzi msirudi nyuma” amesema Profesa Ndalichako.
Ameongeza
kuwa suala la kujenga,kukuza na Kusimamia maadili siyo jukumu la Rais
peke yake au tasisi moja tu,viongozi wa Dini na jamii nzima hivyo sote
tunapaswa kushirikiana kwa pamoja katika ngazi zote kuanzi mashuleni
hadi mtaani.
Amasema
kuwa jamii yetu imeshuhudia katika kipindi hiki kuwepo kwa viashiria
vingi vinavyoonyesha kuporomoka kwa maadili kama hivyo dalili sio njema
hata kidogo kwa mstakabali mzuri wa Taifa letu.
Alimaliza
kwa kusema kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu hufundishika na Yule asiyetii
hawezi kufundishika kwa kuwa hawawezi kusikiliza anachofundishika kwa
kuwa hawezi kusikiliza anachofundishwa na Mwalimu ambaye ndio chachu ya
mafanikio yake kitaaluma.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akiwa
ameongozana na Mkurugenzi mkuu wa Tasisi kupambana na kuzuia Rushwa
(TAKUKURU), Valentino Mlowola kuingia katika ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa Dar es Salaam.
Waziri
wa elimu na mafunzo ya ufundi ,Profesa Joyce Ndalichakoakizungumza
wakati wa ufungzui wa madahalo wa kuhusu maadili kwa wanafunzi.
baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wakifatilia kwa makini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni