Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ally Hapi
amemuagiza Murugenzi wa Halmashauri Ya Wilaya ya Kinondoni Kumsimamisha kazi
Mratibu wa mradi wa TASAF wa wilaya hiyo Onesmo Oyango kutokana ni ubadhilifu
wa fedha za serikali kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa.
Akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa kutoa maagizo hato, Hapi amesema kuwa mratibu huyo aliweza kutoa
fedha taslimu kiasi cha milioni 266 kwa kaya 537 ambazo hazijulikani makazi
yake na milioni 180 kwa kaya 517 ambazo hazistahili kupewa kutokana na kutokuwa
na vigezo ikiwemo kuwa na uwezo wa kujikimu kimaisha na wengine ni wafanyakazi
wa serikalini.
Hapi amesema, jumla ya kaya 1397 hawana
sifa za kupatiwa fedha hizo za mradi wa TASAF ambazo ni mali ya serikali na
zaidi inawataka TASAF kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale ambazo hawakuwa
na vigezo pamoja na kuzitaka kaya hizo kurudisha fedha zote walizozichukua
katila vipindi saba tofauti.
"Kama kutakuwa na njia zozote za
rushwa na udanganyifu wowote katika utoaji wa fedha hizi kwa kaya ambazo hazina
vigezo na zingine hazijulikani zilipo basi jeshi la usalama la Polisi na
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa zihusike mara moja kwa kuwakamata
wahusika waliofanikisha ubadhilifu huo kuanzia kwa Mwenyekiti wa serikali za
mitaa kwani yeye ndo wa kwanza anayewajua wakazi wake,"amesema Hapi.
Hapi amesema kuwa mbali na kaya ambazo
hazikustahili kupatiwa fedha hizo, zipo zingine ambazo zinastahili ingawa
hazijulikani zilipo na nyingine zimehama kutoka wilaya ya Kinondoni.
Hayo
yamegundulika baada ya Mkuu huyo wa wilaya kufanya ziara katila baadhi ya
maeneo na kukuta hali hiyo na tayari ametoa agizo mchakato wa kuwapatia fedha
kaya zinazostahili uanze mara moja na kwa umakini mkubwa na kuvitaka vyombo vya
usalama kushirikiana nao ili haki iweze kutendeka.
Mkuu wa wilaya wa Kinondoni Ally Hapi
(katikati) akitoa taarifa ya ubadhilifu wa fedha katika mradi wa TASAF wilaya
ya Kinondoni na kuamrisha Mratibu wa wilaya hiyo kusimamishwa kazi ili kupisha
uchunguzi, kushoto ni Naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Dennis Manumbu na kulia ni OCD wa Kituo cha Polisi
Magomeni.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni