Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimesitisha uzalishaji kutokana kuelemewa
na gharama za uendeshaji hatua inayowaacha watumiaji wake njia panda.
Mwezi uliopita Kiwanda hicho kilililamikia Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini Tanzania(TPDC) kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati
inazalishwa mkoani Mtwara.
Pia kiwanda hicho kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda
chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya
Liganga ambayo yapo chini ya kiwango na bei ghali.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni