Kurasa

Jumatano, 19 Septemba 2018

YANGA KUIVAA COASTAL UNION YA ALIKIBA ‘MECHI NYINGINE ZA LIGI KUU TANZANIA LEO SEPTEMBA 19,2019 RATIBA IPO HAPA’

Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo kwenye viwanja Sita nyasi kuwaka moto macho ya wapenda soka yatakuwa mji ya Dar es salaam pamoja na Musoma mkoani Mara
Jijini Dar es Salaam mabingwa wa kihistoria katika ligi, Yanga, watakuwa wanacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga, mechi ikianza saa 1 jioni.
Kuelekea mechi hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kipute hicho dhidi ya wagosi wa kaya.
Aidha, katika Uwanja wa Samora huko Iringa, Lipuli itakuwa inaikaribisha Alliance School ya mwanza ambapo mechi itaanza majira ya saa 8 mchana.
Pia kunako dimba la Mwadui Complex wenyeji ambao ni Mwadui FC watakuwa wanacheza dhidi ya JKT Tanzania kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hizi zote zitaruka hewani kupitia Azam TV
Mechi zingine ni
Biashara United vs Azam FC
Mbeya City vs Ruvu Shooting na
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni