Na.Alex Sonna
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho klabu ya Yanga imejitoa rasmi kwenye mbio za kuingia hatua ya robo Fainali baada ya kupigwa magoli 4-0 dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Kenya Gor Mahia mchezo uliopigwa uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi.
Gor Mahia waliweza kuwazidi Yanga kila idara hadi Timu zinakwenda Mapumziko wageni walikuwa hawajapiga shuti lolote kwa wenyeji Jacques Tuyisenge na Ephram Guikan waliweza kuifungia mabao mawili.
Kipindi cha Pili Yanga waliendelea kupotea kwa kila Idara na kushindwa kuipenya ngome ya Gor Mahia beki wa Pembeni Mwinyi Haji alijifunga na kuwaandikia wenyeji bao la tatu kabla ya Ephram Guikan kuandika bao la nne huku yeye mwenyewe akiingia kambani mara mbili.
Mechi nyingi ya kundi D wenyeji Rayon Sports wameshindwa kutamba nyumbani baada ya kuchapwa magoli 2-1 dhidi ya MC Alger toka nchini Algeria.
Yanga hii ni mechi ya pili kupigwa 4g baada ya Mchezo wa kwanza kutandikwa magoli 4-0 dhidi ya MC Alger na mchezo wa pili ililazimishwa sare ya 0-0 uwanja wa Taifa na Rayon Sports kwa matokeo hayo Yanga inamaliza mzunguko wa kwanza bila ya kupata ushindi katika Michuano hiyo.
Kwa Matokeo hayo MC Alger wanaongoza kundi D wakiwa na alama 7,wakifuatiwa na Gor Mahia 5 ,nafasi ya tatu Rayon Sports kwa 2 huku Yanga wakishika nafasi ya mwisho kwa alama 1

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni