
Wizara ya Maliasili na Utalii itashiriki Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar–es-Salaam (SabaSaba) yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2018.
Wizara inawakaribisha wananchi wote na inawajulisha kuwa wale watakaopenda kutembelea Bustani ya wanyamapori hai kutakuwa na kiingilio cha Shilingi 1,000/= kwa watu wazima na 500/= kwa watoto. Gharama hizo za viingilio ni kwa ajili ya kuchangia gharama za utunzaji wa Wanyamapori katika kipindi cha maonesho. Malipo hayo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
Simu ya mkononi.
- Ingia playstore pakua app ya MNRT Portal, jisaliji, chagua kuona wanyamapori wakati wa sabasaba, chagua njia ya kulipa (tigo pesa,mpesa na maxmalipo) chagua kipengele huduma ya malipo ya serikali, lipa kisha utapokea ujumbe kwenye simu na utatumia kama tiketi yako wakati wa kuingia bustanini.
- Ingia www.mnrt.go.tz, (MNRT portal) utaona sehemu ya kuingiza namba ya simu, chagua huduma unayoitaka, andaa bill yako-idadi ya watu utakaokuwa nao (watoto na watu wazima ), lipia bill yako, print risiti yako.
Aidha, unaweza kulipia kiingilio hicho ndani ya Banda la Wizara.
Pia kutakuwa na safari katika Utalii wa jiji la Dar es Salaam, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi pamoja na Msitu Asilia wa Amani.
Njoo ujionee wanyamapori hai, upate elimu kuhusu uhifadhi wa wanyamapori, Misitu, Malikale, Ufugaji Nyuki na uendelezaji Utalii.“Njoo tutalii, tukuze Utalii wa ndani”.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
26/6/2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni