Wanafunzi 150 wa vyuo na vyuo vikuu jijini Dar es salaam leo wamejiunga na CCM na kupokelewa na katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole.
Hayo yamefanyika leo katika darasa la Itikadi la wanachama na wanachama wapya kutoka vyuo na vyuo vikuu.
Akizungumza katika darasa hilo la Itikadi lililofanyika wilaya ya Ilala Ndugu Polepole amewaasa wanachama kuiishi imani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa na nidhamu ya chama na kuendelea kushughulika kuzitatua shida za watu
“Sifa ya chama bora ni kufanyia kazi malalamiko na changamoto hasa za wananchi waliotupatia dhamana” alisema Ndugu Polepole.
Ndugu Polepole ametumia hadhara hiyo kuwakumbusha wanaCCM juu ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kwenye Majimbo ya Siha na Kinondoni kuwa ni maamuzi yaliyozingatia katiba, kanuni, miongozo, taratibu na maslahi mapana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Huu ni muendelezo wa ziara za ujenzi wa chama kwa makundi mbalimbali ya kijamii yenye lengo la kuufikishia umma wa wanachama elimu ya uanachama, umuhimu wa ujenzi wa chama, mageuzi ya Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015 – 2020.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni