Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wafuasi wa upinzani ya Kenya ya National Super Alliance (NASA) wamefanikiwa kugundua mizinga ya nyuki iliyokuwa imetegwa kwenywe uwanja wa Uhuru Park, walipopanga kufanya tukio la kumuapisha Raila Odinga kuwa Rais wa Kenya.
Picha za video zilizooneshwa na kituo cha runinga cha KTN nchini humo zimeonesha wafuasi hao wa Raila ambao wameanza kumiminika katika uwanja huo tangu alfajiri wakichoma baadhi ya mizinga iliyokuwa imefichwa nyuma ya miti, huku wakiendelea kutafuta kama kuna mizinga mingine.
Leo, jiji la Nairobi na Kenya kwa ujumla itashuhudia kitakachotokea wakati wafuasi wa NASA wanapojaribu kufanya tukio la kumuapisha Raila katika uwanja huo ambao tayari jeshi la polisi limeshakataza watu kukusanyika hapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni