Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji
kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi
Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib A. Shariff Mashine 6 za uchunguzi wa
Dawa kutoka Ujerumani kwa kupitia mradi wa EAC, MRH Projat.
rofessa. Richard Jahnke kutoka
Ujerumani akitoa maelezo ya matumizi ya vifaa vipya vya uchunguzi wa
dawa (Minilab Kid) kwa washiriki wa mafunzo ya siku 5 ya uchunguzi wa
dawa kutoka nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika Mbweni.
Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi
wa dawa kujua kuwa ziko salama kwa matumizi ya binadamu wakiwa katika
mafunzo ya vitendo yaliyofanyika katika Kitivo cha Madaktari cha Chuo
Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji
kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi
cheti mshiriki wa mafunzo hayo, Hidaya Juma ambae ni Mratibu wa Mradi wa
uwiano wa udhibiti wa dawa wa nchi za Afrika Mashariki ambae pia ni
Mfamasia kutoka Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.
Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi
wa Dawa kujua kama ipo salama kawa matumizi ya binadam kutoka nchi
wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi
wao na walikwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni