Kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wimbi la migogoro ya ardhi kila kukicha
katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kati ya jamii ya wakulima
na wafugaji na kupelekea wakati mwingine kuibuka kwa mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe ambayo yanasababisha hali ya uvunjifu wa amani na baadhi ya
viongozi na wananchi wengine kupoteza maisha kikatili kimeundwa kikosi
kazi maalumu kwa ajili ya kuweza kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Matukio
ya namna hiyo katika Mkoa wa Pwani yanaonekana kumsikitisha na
kumlazimu Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati sakata
hilo kwa kutangaza rasmi kupambana vilivyo na watu wote ambao
watabainika wanajihusisha na vitendo hivyo vya mauaji ili waweze
kukamatwa haraka na kuweza kufikishwa katika vyombo vya dola ili iwe
fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Waziri
nchemba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea askari
polisi, magereza, uhamiaji pamoja zimamoto wa Mkoani Pwani kwa ajili ya
kuweza kukagua shuguli mbali mbali za utekelezaji ya majukumu yao ya
kila siku ikiwemo na kuweza kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na
kuweka mikakati kwa ajili ya kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
“Kumekuwepo
katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna baadhi ya viongozi wa
vijiji pamoja na wakulima na wafugaji kupoteza maisha, kwa hili sisi
kama Wizara hatuwezi kulivumilia hata kidogo kwani kwa sasa tumejipanga
ii kuweza kuwabaini watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo,”alisema
Waziri.
Alisema
kuwa anasikitishwa kuona mauaji yanafanyika kitu ambacho ni kinyume
kabisa na sheria na taratibu za nchi, kwa mwananchi yoyote kuamua
kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo vya mauaji hivyo
ameahidi kulivalia njuga suala hilo na wale wote watakaobainika wataweza
kuchukuiwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hiyo.
Aidha
Waziri Nchemba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa wahamiaji haramu
ambao wanaingia nchini bila ya kuwa na vibali Wizara yake imeweka
mikakati kabambe ya kuongeza doria usiku na mchana katika sehemu mbali
mbali ikiwemo mipaka, fukwe za bahari pamoja na bandari bubu amabzo
zimekuwa zikitumika kuwapitisha raia hao wa kigeni.
“Tatizo
lawahamiaji haramu katika Mkoa wa Pwani bado ni tatizo kubwa kwani
imekuwa ndio kama lango la kuingilia pindi wanapokuja hasa katika maeneo
ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Wilaya ya Kibaha, hivyo sisi katika
hili tumeshajipanga ili kuweza kuthibiti njia zote ambazo wamekuwa
wakizitumia katika kupita,”alisema Nchemba.
Pia
katika hatua nyingine Nchemba alitoa wito kwa wananchi wote
kushirikiana bega kwa began a serikali pamoja na vyombo vya dola katika
kuwabaini na kuwafichua watu ambao wanakuwa na mashaka nao kwani wengine
wanaingia nchini kwa ajili ya kufanya matukio mbali mbali ya uharifu wa
kutumia siraha.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ameiomba serikali ya awamu ya tano kupitia
Wizara
ya mambo ya ndani kuhakikisha inaongeza vitendea kazi pamoja na
kuongeza ujenzi wa vituo vingine vidogo vya polisi ambavyo vitaweza
kusaidia kuimarisha hali ya ulinzi na usalama pamoja na kupamba na
waharifu ambao wanaingia Mkoa wa Pwani kinyemela na kujificha.
Pia
Koka alimwomba waziri wa mambo ya ndani kuweka utaratibu wa kuhakikisha
vituo vidogo vya polisi vilivyojengwa vinakuwa wazi wakati wote lengo
ikiwa ni kuweza kupambana na matukio mbali mbali ya uharifu ambayo
yanakuwa yanajitokeza bila ya kuwa na muda maalumu hivyo vituo vikiwa
wazi kutaweza kusaidia kupunguza hali ya uharifu.
Matukio
ya vitendo vya mauaji katika baadhi ya maeneo Mkoani Pwani ambayo
yanawahusisha wakulima na wafugaji pamoja na baadhi ya viongozi wengine
bado yanaonekana kuwa ni tishio na kuendelea kufanyika hivyo
kunahitajika jitihada za makusudi zifanyike kutoka serikalini ili kuweza
kutatua migogoro hiyo na kurudisha hali ya amani na utulivu kwa
wananchi.
Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mbunge wa
Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakizungumza jambo baada ya
kulikagua gari ambalo lilikamatwa likiwa na wahamiaji haramu 150
Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambao ni raia wa Ethiopia.
Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wa kulia na kushoto kwake ni
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakiangalia gari ambayo
ilikamatwa Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ikiwa na wahamiaji haramu
wapatao 150 ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia ambao walikamatwa
wakati wakiwa wapo safari kuelekea miko ya kusini.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni