Kurasa

Alhamisi, 15 Desemba 2016

WAZIRI JANUARI MAKAMBA AMELITAKA BARAZA LA WAFANYAKAZI LITUMIKE KUTATUA MIGOGORO YA WAFANYAKAZI

Tawi la baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya makamu wa Rais limetakiwa kuwa ndio sehemu sahihi ya kujadili na kutatua migogoro ya wafanyaki na siyo majukwaa ya siasa.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba, Lipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini dar  es Salaam.

 Mhe.Makamba alisema kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu wajumbe kukaa pamoja kujadili masuala ya msingi yanyowahusu watumishi kwani wao ndo waliowachangua hivyo, majadiliano yanayokuwepo  katika vikao hivyo ni nyenzo muhimu ya kuondoa migogoro na migomo mahala pa kazi.
“Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu, katika kuamua na kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuleta ufanisi na utulivu ndani ya Ofisi yetu.alisisita Makamba”.

Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba, Lengo la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa  kuelekezana, kushauriana na kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi  na ushiriki wa wafanyakazi katika kuyatekeleza na kuyasimamia, na aliongeza kwa kusema kuwa  ni fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa kazi na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.
Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi cha Ofisi ya makamu wa Rais kimudhuriwa na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa na Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar.


one
Katikati Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rias Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Makamu wa Rais leo Jijini DSM kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Professor Faustine Kamuzora na kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Isaya Kisiri.


one-2
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais wakiimba kwa pamoja wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni