Kurasa

Jumanne, 18 Oktoba 2016

MGODI WA KITUNDA TABORA WAPIGWA FAINI YA MILIONI 14 KWA KUENDESHA SHUGHULI ZA UZALISHAJI BILA KIBALI



Serikali imeupiga faini ya shilingi milioni kumi na nne,mgodi wa Kitunda Gold Mining uliokuwa ukifanya shughuli za uzalishaji bila kibali maalumu tangu mwaka 2009,ikiwa ni pamoja na kusababisha uharibufu wa mazingira,na fedha hizo zilipwe ndani ya siku 14 ndipo waendelee na uzalishaji huo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amechukua hatua hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mgodo huo wa Kitunda akiwa na maafisa wa baraza la udhibiti wa mazingira,na kubaini shughuli za uzalishaji zikiendelea kinyemera huku kukiwa hakuna vibali vyovyote.
 
Aidha katika hatua nyingine mhe Naibu Waziri Luhaga Mpina amepiga marufuku wananchi na wawekezaji kuchimba madini ya aina yoyote katika hifadhi za serikali akidai kuwa,sehemu zilizotengwa kwa ajili ya hidfadhi ziheshimuwe,na hatua kali zichukuliwe kwa atakayebainika kukiuka maagizo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni