Kurasa

Ijumaa, 30 Septemba 2016

TAOMAC Wamkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Tsh milioni 404.8 kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Kagera.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wane kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta (TAOMAC) baada ya kupokea hundi ya fedha kiasi cha sh. Milioni mia nne na nne na laki nane (404,800,000) pamoja na mifuko ya simenti 1000 kutoka chama hicho kwa ikiwa ni mchango wa wanachama wa chama hicho kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera. Wengine ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Charles Mwijage (wa kwanza kulia).



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea fedha kiasi cha sh. Milioni mia nne na nne na laki nane (404,800,000) pamoja na mifuko 1000 ya simenti kutoka kwa Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta TAOMAC ikiwa ni mchango wa wanachama wa chama hicho kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera,Tanzana


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni