Hofu ya kutokuwapo usalama ndani ya ofisi kuu za CUF Buguruni,
imesababisha kuahirishwa mapokezi ya viongozi wakuu wa chama hicho.
Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya
chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini
yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu.
Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki
Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa
wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama
siyo nzuri.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni